KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 5, 2010

Wanasiasa waomba watumia lugha za asili kwenye kampeni

WANASIASA wa vyama mbalimbali nchini jana waliwasilisha ombi kwa Tume ya Uchaguzi (NEC) kutaka waruhusiwe kutumia lugha za asili za makabila yao wakati wa kampeni wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.Ombi hilo waliwasilisha kwenye mkutano uliowakutanisha wanavyama mbalimbali wa siasa uliofanyika jijini Dar es salaam uliokuwa na lengo la kujadili rasimu ya maadili ya uchaguzi.

Ombi hilo ambalo lilikuwa vutio la wanasiasa wengi na lilileta mjadala mzito ndani ya mkutano huo uliowakutanisha wanasiasa hao.

Waliwasilisha ombi hilo kwa tume hiyo baada ya mkurugenzi wa Nec, Bw. Rajab Kiravu kutoa mwongozo mzima wa jinsi kampeni hizo zitakavyoendeshwa na na uchaguzi kwa ujumla ambapo katika mwongozo huo ulionyesha kuwa Kiswahili pekee ndicho kitakachoruhiwa kutumika kaika kampeni hizo.

Kipengele hicho cha 2.1 (k) cha rasimu kilisema kuwa “Kiswahili itakuwa ndiyo lugha pekee katika kampeni za Uchaguzi, na endapo itatokea lugha hiyo ya Kiswahili haitaeleweka eneo husika basi mgombea atazungumza Kiswahili na mkalimani ataruhusiwa kutatafsiri katika lugha inayoeleweka katika eneo hilo” kilisme akipengele hicho

Hivyo mara baada ya kusoma kipengele hicho wanasiasa hao wakazusda mjadalda mkubwa kuhusiana na kukatazwa kugha za makabila kwenye mikutano na kuwasilisha ombi hilo upya kwa tume hiyo ili lugha hizo ziweze kutumika ili wananchi wao waweze kuwaelewa kwa undani zaidi.

Hata hivyo mjadalda huo haukuzaa matunda kwa makubaliano NEC ilipanga tarehe nyingine ya kujadili suala hilo.

Katika Mkutano huo vyama vilivyohudhuria CUF, NLD, CHADEMA, TLP, NCCR, SAU, TADEA na AFP.

No comments:

Post a Comment