KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 5, 2010

Rio Ferdinand nje ya timu ya England


Nahodha wa England Rio Ferdinand atakosa Kombe la Dunia baada ya kuumia goti katika mazoezi ya mwanzo nchini Afrika Kusini.

Ferdinand amepumzishwa kwa takriban wiki nne mpaka sita ikiwa kano ya goti lake la kushoto limepata jeraha.

Mlinzi wa klabu ya Tottenham Michael Dawson atasafiri siku ya Ijumaa kuziba nafasi ya Ferdinand, huku Steven Gerrard akichukua nafasi yake ya nahodha.

No comments:

Post a Comment