KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, June 2, 2010

Mauaji ya Libya yalaaniwa


Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limelaani mauaji ya watu 18 yaliyofanyika nchini Libya.

Vyombo vya habari vya Libya vimeripoti kuwa watu hao 18, wengine kutoka Chad, Misri na Nigeria, waliuawa siku ya Jumapili mjini Tripoli na Benghazi.

Amnesty International imesema inahofia washutumiwa hao hawakutendewa haki.

Gazeti la Cerene la Libya limesema, watu hao walikuwa wanashtakiwa kwa makosa ya mauaji na kuuawa kwa kupigwa risasi.

Tamko kutoka shirika hilo limesema, " Huko Libya tunahofia hukumu za vifo hutolewa baada ya kushindwa kuendesha kesi katika viwango vya kimataifa."

Amnesty imesema, raia wa kigeni hawatendewi haki katika mfumo wa sheria wa Libya.

Aghlabu hawana uwezo wa kupata mawakili na hawaelewi kesi hizo zinavyoendeshwa kutokana na kutumia lugha ya kiarabu.

Amnesty imesema, Libya hutoa idadi kubwa ya hukumu za kifo kwa raia wa kigeni.

Kila mwaka maelfu ya wahamiaji wa Afrika husafiri katika jangwa la Sahara kuelekea Libya kwa matumaini ya siku moja kufika Ulaya.

No comments:

Post a Comment