KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, June 18, 2010

Nyumba ya vyumba 17 Yateketea Kwa Moto Tabata


MOTO ulioanza katika chumba cha biashara kinachojishughulisha na uuzaji wa vipodozi ulisababisha nyumba vingine 16 kuteketea kwa moto na hakuna kilichookolewa huko maeneo ya Tabata Shule jijini Dar.
Moto huo ulianza kwenye majira ya saa 3 asubuhi ulienea nyumba nzima kwa kile kilichosemekana kuchelewa kwa gari la zimamoto kuokoa nyumba hiyo.

Moto huo ulizuka ghafla kwa kile kilichodaiwa ni hitilafu ya umeme ulioanza katika duka hilo la vipodozi.

Mmiliki wa nyumba hiyo bi.Sabitina Kandege alisema nyumba yake ilikuwa na vyumba 12 na vyumba vya maduka vitano vyote kwa pamoja viliteketea kwa moto na kupoteza mali zilizokuwa kwenye vyumba hivyo.

Wakati huohuo sehemu ya soko la Kariakoo imeteketea baada ya moto kuzuka na kusababisha wafanyabiasha kutandwa na hofu na kusimama kwa shughuli zao kwa masaa kadhaa.

Moto huo ulizuka saa 12 asubuhi katika ofisi ya kuhifadhia silaha na kuteketeza baadhi ya nyaraka muhimu za ofisi za soko hilo.

Wakati moto huo ulipoanza kutanda sokoni humo wafanyabiasha walikuwa katika hofu kubwa ya kupoteza mali zao kwa kuwa wezi na vibaka walishakuwa tayari kuiba mali za wafanyabiasha hali iliyofanya halmashauri ya jiji kuagiza zaidi ya wanagambo 30 waliokuwa na virungu kuja kudhibiti hali ya ualama sokoni hapo.

Hata hivyo Kikosi cha Zima Moto Cha Halmashauri ya Jiji kiliwahi kufika na kumaliza moto huo ambao ungeweza kuliteketeza soko hilo.

Meneja wa soko la Kariakoo Florence Seiya alipoulizwa chanzo cha moto huo, alisema chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika mara moja na kusema huenda ikawa ni hitilafu ya umeme ndani ya chumba hicho cha kuhifadhia silaha ambacho hakifunguliwi mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment