KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, June 18, 2010

Askari Waliowalazimisha Wanawake Kunyonya Sehemu Zao Za Siri Kukiona –Pinda


WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda jana aliomba radhi kwa niaba ya serikali kufuatia tukio lililoripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa kuna askari polisi waliwadhalilisha wanawake kwa kuwavua nguo na kisha kuwalazimishwa kuwanyonya sehemu zao za siri.
Kufuatia tukio hilo Waziri Pinda aliwaomba radhi wananchi wote kwa ujumla na kuelezea kusikitishwa na vitendo hivyo vya askari polisi walivyowafanyia wanawake hao kwa kuwa ni kinyume na utendaji wa jeshi hilo.

“Kwanza naomba niombe radhi iwapo tukio hili la aibu ni kweli limefanywa na askari polisi kwa sababu si jambo la kawaida katika jamii ya watanzania, polisi kuweza kufanya kitendo cha udhalimu wa namna hiyo. Nasema kama ni kweli watakiona “, alisema Pinda.

Pinda alisema jana Bungeni kuwa atahakikisha askari waliohusika katika vitendo hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Pinda aliyasema hayo baada ya kufuatia kuulizwa swali la papo kwa papo na mbunge wa Tarime [Chadema] Charles Mwera kutaka kujua ni hatua gani zinachukuliwa na serikali kufuatia vitendo hivyo vilivyofanywa na askari hao.

Pinda alijibu hayo na pia kumuahidi mbunge huyo kukutana naye mara baada ya kikao hicho cha bunge ili atoe maelezo kiundani kuhusu madai hayo na kumuagiza Waziri wa Mambo ya ndani wawe nae katika mazungumzo hayo.

Mbunge huyo alisema kuwa kuna baadhi ya askari polisi mkoani Mara waliwakamata wanawake na kuwaamuru wawavue nguo zao na kisha kuwaamrisha kuchezea nyeti za askari hao kabla ya kuwalazimisha kuzinyonya nyeti hizo.

Swali la mbunge huyo kwa Waziri Mkuu liliwaacha wabunge wengi vinywa wazi wasiamini kama kweli mambo haya yanafanyika Tanzania

No comments:

Post a Comment