KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, June 18, 2010

Afa kwa kukanyagwa na gari baada ya kuanguka na pikipiki


KIJANA mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 29 hadi 30 amefariki dunia papohapo baada ya kukanyagwa na gari aina ya LandCruiser alipoanguka na pikipiki huko maeneo ya Bigbrother njia panda ya Mabibo.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya usiku, katika kona hiyo baada ya kijana huyo kutaka kuingia kona ya Mabibo na kushindwa na kuanguka kwa kuwa alikuwa kwenye mwendo kasi na papohapo gari hilo lililokuwa likitokea Manzese kwenda Ubungo lilimkanyaga.

Gari hilo lilimkanyaga wakati kijana huyo akitafuta mbinu za kuinuka kwa kuwa alijijeruhi na kabla hajafanya hivyo gari hilo bila kutambua lilishindwa kufunga breki na kumkanyaga na kupelekea kifo chake.

Mwili wa kijana huyo ulichukuliwa na ulipelekwa hospitali kuhifadhiwa.

Katika tukio jingine la aina hiyo, Koku Chungu (22), amekufa papohapo baada ya kugongwa na gari aina Mercedes Benz wakati yeye akiwa anaendesha baiskeli.

Koku alikuwa akiendesha baiskeli akitokea Sinza Madukani kwenda Mapambano na ghafla aligongwa na gari hilo lililokuwa na namba T 603 lililokuwa likiendeshwa na Richard Kabaraga [55] na kufa papohapo

Akitoa taarifa juu ya tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, amesema tukio hilo lilitokea jana, majira ya saa 11 jioni, katika barabara ya Nzasa, Sinza Mapambano.

Maiti imehifadhiwa chumba cha maiti Hospitali ya Mwananyamala na Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi

No comments:

Post a Comment