KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, June 18, 2010

Ndoa ya Wanaume Waliooana Malawi Yavunjika


Wanaume wawili wa nchini Malawi ambao ndoa yao ilisababisha watupwe jela miaka 14 kabla ya rais wa Malawi kuingilia kati na kuamuru waachiwe huru, ndoa yao imevujika ndani ya wiki mbili baada ya kuachiwa huru.
Mashoga wa malawi ambao walisamehewa adhabu yao ya kifungo cha miaka 14 jela kwa kuendeleza tabia ya Sodoma na Gomora, ndoa yao imevunjika ikiwa ni miezi sita baada ya harusi yao.

Steven Monjeza, 26, na Tiwonge Chimbalanga, 20, walitiwa mbaroni mwezi disemba mwaka jana baada ya kufanya sherehe za harusi mjini Blantyre kusherehekea kuoana kwao.

Kukamatwa kwao kulisababisha shinikizo kubwa kwa haki za mashoga nchini Malawi, walihukumiwa kwenda jela miaka 14 lakini rais Bingu wa Mutharika alitengua adhabu hiyo mei 29.

Ndani ya wiki mbili baada ya kuachiwa huru Monjeza ametangaza kuwa uhusiano wake na "mkewe" Chimbalanga umevunjika.

"Sina tena uhusiano wa kimapenzi na Tiwonge Chimbalanga, nimeangukia kwenye mapenzi na mwanamke anayeitwa Dorothy Gulo,", alisema Monjeza akiongea na shirika la habari la AFP.

"Tunapanga maisha ya baadae na Dorothy", aliongeza Monjeza.

Chimbalanga kwa upande wake alisema kuwa amezisoma habari za kuvunjika kwa ndoa yake kwenye magazeti.

"Sijahuzunika na chochote kuhusiana na hili", alisema Chibalanga na kuongeza "Monjeza yuko huru kumuoa yoyote ampendaye kama vile ambavyo mimi nitaolewa na mwanaume atakayekuwa kipenzi cha maisha yangu, kuna wanaume wazuri wengi kila kona, nitaendelea kuwa shoga".

"Kitu ambacho ningependa mjue ni kwamba hakuna mtu aliyemlazimisha kufunga ndoa na mimi mwezi disemba mwaka jana", aliongeza Chimbalanga.

Chimbalanga alisema kuwa Monjeza amekuwa akishinikizwa na ndugu zake atafute mpenzi mwanamke.

Mjomba wake Monjeza, Khuliwa Dennis Monjeza,alisema kuwa atahakikisha kuwa Chimbalanga hafanyi chochote ili kumnasa tena Monjeza.

Akiongea kuhusu kumrudia Chimbalanga, Monjeza alisema kuwa amejifunza kwa kipindi cha miezi mitano aliyokaa jela hivyo asingependa tena kujihusha na mahusiano ya jinsia moja

No comments:

Post a Comment