KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, June 18, 2010

Mashoga Milioni 3 Waandamana Brazili Kudai Haki Zao


Mashoga na wasagaji milioni 3 wanaandamana mjini Sao Paulo nchini Brazili kudai haki zao za kutambulika na kukubalika katika jamii.
Mamilioni ya wanawake wasagaji na wanaume mashoga wanaandamana kwenye mitaa maarufu ya Sao Paulo Brazili kudai haki zao.

Wakiwa wamevalia nguo za rangi mbalimbali, mashoga na wasagaji wanaandamana kulaani watu wanaopinga uhusiano wa jinsia moja.

Waandamanaji hao pia wanataka mashoga na wasagaji wasitengwe katika jamii na wapewe haki sawa na watu wengine.

Mwaka jana pekee, jumla ya mashoga 198 waliuliwa nchini Brazili na watu ambao wanapinga mahusiano ya kimapenzi baina ya watu wa jinsia moja.

Waandaaji wa maandamano hayo wanakadiria jumla ya mashoga na wasagaji milioni 3.2 wamehudhuria maandamano hayo ambayo yamegeuka kuwa kivutio cha watalii.

Maandamano ya mwaka huu yamedhaminiwa na kampuni ya mafuta ya Petrobras inayomilikiwa na serikali

No comments:

Post a Comment