KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, June 18, 2010

Bibi Aokoa Mbwa Toka Kwenye Moto, Amsahau Mjukuu Wake


Bibi mmoja nchini Uingereza alikumbuka kuwaokoa mbwa wake wanne toka kwenye nyumba yake iliyokuwa ikiwaka moto lakini alisahau kumuokoa mjukuu wake aliyekuwa amelala ndani ya nyumba hiyo.
Mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 11 alisahaulika ndani ya nyumba iliyokuwa ikiwaka moto wakati bibi yake alipokuwa bize kuwaokoa mbwa wake.

Bibi huyo wa nchini Uingereza, Mandy Hands, 45, alisahau kuwa mjukuu wake alikuwa amelala ndani ya nyumba hiyo wakati alipokuwa bize kunusuru maisha ya mbwa wake wanne.

Zimamoto waliowahi kufika kwenye eneo la tukio, walifanikiwa kumuokoa mtoto huyo.

Mandy anasema kuwa anajuta kumsahau mjukuu wake kwenye moto. "Najisikia vibaya nikikumbuka nilimsahau mjukuu wangu kitandani moto ulipotokea".

"Alikuja kututembelea toka Portsmouth na kwasababu ya kupaniki nilisahau kuwa yuko hapa", alisema Mandy.

Moto huo ulizuka jumatatu asubuhi kutokana na hitilafu ya umeme. Mandy baada ya kuona moshi ukiingia chumbani kwake alifanikiwa kumuamsha mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 16 na ndipo alipoanza kuwaokoa mbwa wake wanne.

Aligundua amemsahau mjukuu wake ndani ya nyumba hiyo wakati akiwa nje zimamoto walipomuuliza kama kuna mtu yoyote ndani ya nyumba hiyo.

Zimamoto walifanikiwa kumtoa mtoto huyo toka kwenye nyumba hiyo akiwa hana majeraha yoyote ya moto

No comments:

Post a Comment