KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, June 10, 2010

6 wafa, 29 wajeruhiwa kwenye ajali Zanzibar


WATU sita wamefariki dunia na wengine 29 kujeruhiwa baada ya gari ya abiria waliyokuwa wakisafiria kuangukiwa na gari la kubebea maji katika ajali iliyotokea jana huko eneo la Koani, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja
Gari aina ya Tata lililokuwa na namba T 807 AHC lililokuwa limebeba maji lilishindwa kupanda mlima na kuanza kurudi nyuma kwa kasi na kuliangukia gari la abiria yenye namba za usajili Z 609 AB inayofanya safari zake kati ya Machui na mjini Zanzibar

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Makarani Ahmed, aliviambia vyombo vya habari kuwa, ajali hiyo ilitokea baada ya gari la kubeba maji kufeli kupanda mlima na kuliangukia daladala iliyokuwa na abiria hao.

Akifafanua tukio hilo alisema kuwa kati ya majeruhi hao, 10 ni wanawake, wanaume wanane na 11 ni watoto na kusema wengi wao wamekatika miguu na mikono.

Waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni dereva wa daladala hiyo, Salum Ali Issa (38), Salum Ali Ame (40), Yussuf Abdallah Yussuf (79), Abdallah Maulid Abdallah (6), Shaida Amour Abdallah (27) na Asha Abdallah Saleh (30).

Hata hivyo kamanda huyo alisema dereva wa gari lililosababisha ajali alitoweka mara baada ya ajali hiyo kutokea na juhudi za kumsaka dereva huyo zinaendelea.

Ajali hii ilidaiwa na wakazi wa visiwani humo kuwa ni ajali mbaya ya kwanza kutokea toka mwka huu uanze visiwani Zanzibar na wengi kusikitishwa na tukio hilo.

Makarani alisema majeruhi wa ajali hiyo wote wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment