KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, June 8, 2010

Mikel kutocheza Kombe la Dunia, majeruhi


Kiungo wa timu ya taifa ya Nigeria, John Mikel Obi, ametangaza kujitoa katika michuano ya Kombe la Dunia 2010 huko Afrika Kusini kutokana na majeraha ya goti.

Mikel anaungana na nyota wengine wa Chelsea, Michael Essien na Michael Ballack ambao watakosa michuano hiyo mikubwa kutokana na majeraha, pia kuna wasi wasi kuwa Didier Drogba naye huenda asicheze.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, alifanyiwa upasuaji wa goti mwezi Mei, lakini amesema bado hajisikii kuwa amepona kikamilifu kiasi cha kucheza katika Kombe la Dunia.

"Tumemwondoa Mikel kutoka kikosi chetu baada ya kueleza kuwa asingependa kuhatarisha uchezaji wake," msemaji wa timu ya Nigeria alieleza.

Nafasi yake Obi Mikel itajazwa na Brown Ideye, mshambuliaji kutoka klabu ya Sochaux ya Ufaransa, ambaye hajawahi kuchezea timu ya taifa ya Nigeria.

No comments:

Post a Comment