KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, June 8, 2010

A Kusini yafukuza 'wahuni' wa Argentina


Afrika Kusini imewafukuza wanaodhaniwa kuwa mashabiki wahuni 10 kutoka Argentina ambao polisi wanasema walikuwa na mpango wa kuvuruga Kombe la Dunia.

Watu hao, ambao ni miongoni mwa kundi la mashabiki 80, walikamatwa katika uwanja wa ndege wa Johannesburg na kugundulika kuwa walikuwa katika orodha ya watu waliopigwa marukuku kuingia Afrika Kusini.

Polisi nchini humo wamesema hatua hiyo inaonyesha jinsi gani maandalizi ya usalama kabla ya mashindano hayo yanavyotekelezwa.

Kombe la Dunia, linalofanyika barani Afrika kwa mara ya kwanza-linaanza Ijumaa.

Watu hao wanasemekena kuwa wanachama wa "barras bravas" wa Argentina, makundi yanayojulikana kwa kufanya ghasia katika mashindano ya soka.

Walikamatwa siku ya Jumapili baada ya kusafiri kutoka Argentina kupitia mji wa Luanda nchini Angola, na kuondoshwa Jumatatu.

Kutokana na polisi, takriban wawili miongoni mwao walikuwa viongozi wa makundi hayo, na mwengine alikuwa nje kwa dhamana kutokana na makosa ya mauaji.

No comments:

Post a Comment