KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, June 8, 2010

Idadi ya vifo vyaongezeka Darfur

Takriban watu 600 wamefariki dunia mwezi Mei kutokana na mapigano mjini Darfur nchini Sudan, idadi kubwa kutokea kwa mwezi tangu majeshi ya kutunza amani yalivyosambazwa mwaka 2008.

Jeshi la kutunza amani la muungano wa Umoja wa Mataifa na Afrika limesema wengi walikufa kutokana na mapigano baina ya jeshi la Sudan na waasi wa Justice and Equality Movement (Jem).

Idadi ya waliokufa imeongezeka tangu Jem walipojitoa kwenye mazungumzo ya amani.

Waasi hao walitia saini makubalino ya awali ya amani na kuacha mapigano mwezi Februari.

Hii ina maana kuwa uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi tangu miaka 24 iliyopita uliofanyika mwezi Aprili, ulikuwa kimya sana mjini Darfur.

Lakini Jem walisusia majadiliano hayo mjini Qatar, ikidai serikali ilianzisha mapigano mapya.

Ripoti kutoka jeshi hilo limesema watu 440 walifariki dunia katika mapigano mwezi Mei baina ya waasi na majeshi ya serikali, 126 katika vurugu za kikabila na 31 katika ghasia nyingine, ikiwemo mauaji.


Mgomo 'utaendelea'

Darfur
Nyaraka za siri, zilizoonekana na mashirika ya habari, zimesema makundi mawili hasimu ya kiarabu, Rezeigat na Misseriya, nayo pia yalipambana mjini Darfur tangu mwezi Machi.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, takriban watu 300,000 wameuawa Darfur na zaidi ya milioni 2.6 wamehama makazi yao tangu waasi walipoanza mapigano mwaka 2003.

Hata hivyo, serikali ya Sudan, imesema takwimu hizo zimetiwa chumvi.

Rais wa Sudan Omar al-Bashir anatakiwa na mahakama ya kimataifa ICC kwa madai ya uhalifu wa kivita yaliyofanywa Darfur, mashtaka anayoyakana vikali.

No comments:

Post a Comment