KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 5, 2010

Kimbunga Chalimeza Jengo la Ghorofa Tatu


Mvua na mmonyoko wa ardhi uliosababishwa na kimbunga cha tropiki kinachoitwa Agatha kimesababisha vifo vya watu 120 nchini Guatemala pamoja na jengo la ghorofa tatu kumezwa chini ya ardhi na kusababisha shimo kubwa sana.
Watu 120 wamefariki na wengini 53 hawajulikani walipo baada ya kimbunga Agatha kuitandika Guatemala na nchi kadhaa za Amerika ya Kati.

Katika kimbunga hicho, jengo la ghorofa tatu na nyumba moja ndogo zilimezwa chini ya ardhi na kusababisha shimo kubwa sana.

Vyombo vya habari vya Guatemala vilisema kwamba mlinzi mmoja katika jengo hilo alifariki baada ya kutumbukia kwenye shimo hilo kubwa.

Wakazi wa eneo hilo walisema kuwa mfumo mbovu wa maji taka ndio sababu ya kutokea kwa shimo hilo kubwa.

Mafuriko na mmonyoko wa ardhi uliosababishwa na kimbunga hicho umepelekea watu wengi wakose makazi ya kuishi baada ya nyumba nyingi kuharibiwa na mmomonyoko wa ardhi.

No comments:

Post a Comment