KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, June 5, 2010

Mwanaume mmoja nchini Ireland amejikuta akimzalisha dada yake

Mwanaume mmoja nchini Ireland amejikuta akimzalisha dada yake bila kutarajia baada ya kuangukia kwenye mapenzi bila kujua kuwa mwanamke huyo ni dada yake. Ameamua kufunga naye ndoa ili waweze kumtunza mtoto aliyezaa naye.
Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina la Mark wa nchini Ireland alijikuta akizaa na dada yake wa baba mmoja mama tofauti, baada ya kuanza naye uhusiano bila kufahamu kuwa ni dada yake.

Wazazi wa Mark waliachana wakati Mark akiwa mdogo sana ambapo kwa jinsi ndoa hiyo ilivyovunjika kwa mgogoro mkubwa mahakamani, Mark alipewa jina tofauti la baba na mahakama iliamuru mtoto huyo asiambiwe baba yake anaitwa nani.

Kasheshe liliibuka baada ya Mark kukutana na mwanamke disco katika mji tofauti na anaoishi. Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Maura naye alienda kwenye disco hilo akitoka kwenye mji mwingine tofauti.

Mark alianza uhusiano wa kimapenzi na Maura wakati huo. Miaka miwili baadae Maura alipopata ujauzito ndipo wawili hao walipoamua kuishi pamoja.

Baada ya Maura kujifungua, Mark aliamua kumtambulisha Maura kwa mama yake na ndipo ukweli ulipofichuka.

Mama yake Mark alimuuliza Maura baba yake anaitwa nani, alipolitaja jina lake ndipo mama huyo alipomwambia Mark "Mwanangu huyo ni dada yako".

Matokeo ya vipimo vya DNA yaliyotolewa mwezi uliopita yalithibitisha kuwa Mark na Maura ni mtu na dada yake.

Hata baada kugundua kuwa uhusiano wao ni haramu, wawili hao wameamua kuuendeleza na wamepanga kuzaa watoto wengi zaidi.

"Najua watu watatufikiria vibaya, kama tusingekuwa na mtoto tungeweza kufikiria kusitisha uhusiano wetu lakini kwakuwa tuna mtoto mmoja, tutafunga ndoa tuzae watoto wengi zaidi", alisema Mark.

Mark na Maura wanatoa lawama zao kwa mfumo wa sheria ambao ulizuia Mark kumjua baba yake.

Wamepanga kumfungulia kesi ya fidia jaji aliyeamuru Mark asijulishwe baba yake.

No comments:

Post a Comment