KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, June 5, 2010

‘Wanawake Kuwafundisha Wanaume ni Haramu’


Mwanazuoni wa kiislamu wa nchini Saudi Arabia ameenda mahakamani kupinga serikali kuwaruhusu walimu wanawake kufundisha watoto wa kiume katika shule za msingi kwakuwa wanawake kuwafundisha wanaume ni haramu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Arab News, mtaalamu wa sharia za kiislamu, Youssef al-Ahmad ameenda mahakamani kuweka pingamizi hatua ya wizara ya elimu kuwaruhusu walimu wanawake kufundisha kwenye shule za wavulana.

Youssef alisema kuwa wanawake kufundisha wavulana ni haramu na ni marufuku katika sheria za kiislamu.

Youssef alisema kuwa ameamua kwenda mahakamani baada ya wizara ya elimu kuipuuzia barua aliyowaandikia kuwafahamisha kuwa ni kinyume cha sheria za kiislamu wanawake kufundisha kwenye shule za wavulana.

“Nilipoona sijibiwi chochote ndio nimeamua kwenda mahakamani”, alisema.

Mwezi uliopita, naibu waziri wa elimu Noural al-Fayez ambaye ndiye waziri wa kwanza mwanamke katika historia ya Saudi Arabia, alitangaza kuwa walimu wanawake wataruhusiwa kufundisha kwenye shule za wavulana kuanzia darasa la kwanza hadi la tatu katika shule binafsi pekee.

Youssef anapinga hatua ya kuruhusu wanawake kufundisha kwenye shule za wavulana akisema kuwa huo ni mpango wa nchi za magharibi kulazimisha shule za mchangayiko wa jinsia.

No comments:

Post a Comment