Watafiti kutoka nchini Uingereza na Marekani, wamebaini kuwa wafanyakazi wa migodini Kusini mwa jangwa la Sahara, wanakabiliwa na tisho kubwa zaidi la kuambukizwa ugonjwa wa kifua kikuu, kuliko wafanyakazi wengine kote duniani.
Kulingana na matokeo ya utafiti huo yaliyochapishwa katika jarida la afya ya umma la Marekani, baadhi ya mambo yanayochangia ugonjwa huo ni mazingira duni na makaazi mabovu ya kuishi.
Mambo mengine yanayochangia ugonjwa huo kwa mujibu wa ripoti hiyo , ni vumbi linalotoka kwenye migodi hiyo pamoja na usambazaji wa virusi vya HIV miongoni mwa wafanyakazi.
Wafanyakazi wanaosafiri mwendo mrefu kufanya kazi pia wanakumbwa na tisho la kuambukizwa kifua kikuu kulingana na ripoti hiyo.
No comments:
Post a Comment