Waziri mkuu wa Japan, Yukio Hatoyama, ametangaza kuwa atajiuzulu.
Kura za maoni nchini Japan zinaonyesha kuwa ushawishi wa bwana Hatoyama umeshuka kwa kiasi kikubwa hususuan kufuatia shinikizo za wanchama wake wa chama tawala.
Hii ni baada ya kukosa kutimiza ahadi yake ya kampeini ya kuondoa kambi ya kijeshi ya Marekani Kusini mwa kisiwa cha Okinawa.
Bw. Hatoyama pia anaohofiwa huenda akasabisha chama tawala kushinda kwenye uchaguzi wa waakilishi wa baraza la Senate utakaofanyika mwezi ujao.
Inaarifiwa ahadi ya Bw. Hotayama haikutimia kufuatia shinikizo kutoka kwa Marekani.
No comments:
Post a Comment