SERIKALI ya Tanzania imetenga kiasi cha shilingi bilioni 76 kwa ajili ya ujenzi wa upanuzi wa barabara za Jiji la Dar es Salaam ili kumaliza kero inayowakabili wakazi wa humo kutokana na foleni zinazosababishwa na ufinyu wa barabara.
Hayo yalibainishwa na Waziri wa Miumbombinu, Dk. Shukuru Kawambwa, alipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa mradi huo unaoanza.
Amesema kiasi hicho kilichotengwa na pamoja na kulipw fidia kwa wakazi ambao watabomolewa nyumba zao na kuwaagiza watendaji kufanya tathimini ya mali za wakazi ili gharama za ujenzi huo zisizidi kiasi hicho ambazo zimetengwa.
Amesema wizara yake itahakikisha bajeti ya mwaka wa fedha 2010/2011 itamaliza tatizo hilo kwa lengo ya kupunguza kero ya foleni inayowakabili wakazi wa jiji.
Amesema kutokana na tatizo la foleni kuwa kubwa mno ndani ya jiji na kusababisha wafanyakazi kuchelewa makazini ka kutumia masaa mengi barabarani bajeti hiyo itahakikisha tatizo hilo linapunua ndani ya jiji.
No comments:
Post a Comment