KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, June 5, 2010

Mahakama yaonyesha mkanda wa video jinsi Mtikila alivyomkashifu Rais

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam, imeonyesha mkanda wa video mbele ya waandishi wa habari ulionyesha mkutano uliofanywa na Mchungaji Christopher Mtikila jinsi alivyotoa kashfa kwa kumuita Rais Jakaya Kikwete kuwa ni gaidi.
Katika video hiyo, Mtikila alionekana akihutubia mbele ya waandishi wa habari huku akiwa amevalia suti nyeusi, shati jeupe na tai ya bluu na akisikika akisema kwa kujiamini


“naomba niseme wazi kabisa kuwa Kikwete ni gaidi namba moja wa nchi hii, anaongoza nchi kwa imani yake ya dini na maamuzi ya nchi hii anayatoa kutokana na imani yake hiyo, mimi nasema hatutaweza kuvumilia nchi iongozwe na mhuni kama yeye” haya ni maneno aliyasema na kurekodiwa ndani ya mkanda huo
Kwa kuwa sauti ilikuwa ni ndogo Mtikila alilazimika kusogea karibu na Tv iliyokuwa ikionuyesha mkanda huo mahakamani ili aweze kusikiliza vizuri maneno hayo
Katika hali iliyowashangaza wengi mara bada ya kuwasilishwa kielelezo hicho mahakamani Mtikila alikana kuwa maneno hayo hakuyatoa yeye kwenye kinywa chake.
Awali ilidaiwa kuwa, Oktoba 21, 2007 Mtikila akiwa katika nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Ilala, Dar es Salaam,mkabala na kiwanda cha bia alitoa lugha ya uchochezi wa kuvunja imani ya nchi na kutoa maneno hayo kumkashifu Rais Kikwete.
Mtikila yuko nje kwa dhamana, na Kesi hiyo itarudi tena mhakamani hapo Juni 14, mwaka huu,kwa kuendelea kusikilizwa.

No comments:

Post a Comment