KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, June 18, 2010

Vinywaji, Sigara,Usajili wa Magari imekula kwao

Katika bajeti ya mwaka 2010/11 iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo ilibainisha kuwa vinywaji, sigara na usajili wa vyombo vya usafiri vya moto vimepanda maradufu kwa asilimia 8.
Hatua hiyo imekuja katika katika kuzinazingatia dhamira ya Serikali kukuza viwanda, ajira na mapato ya ndani.

Katika uainisho huo vinywaji baridi ushuru utapanda kutoka Shilingi 58 hadi Shilingi 63 kwa lita, bia iliyotengenezwa kwa nafaka ya nchini na ambayo haijaoteshwa itapanda kutoka Shilingi 209 hadi Shilingi 226 kwa lita, na bia nyingine zote ambazo nafaka hutoka nje ya nchi itatozwa kwa Sh 354 hadi Sh 382 kwa lita moja.

Mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu kutoka nje ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25 ushuru utapanda kutoka Shilingi 1,132 hadi kufikia Shilingi 1,223 kwa lita moja.

Na vileo vikali vitapanda kutoka Shilingi 1,678 hadi kufikia Shilingi 1,812 kwa lita moja.

Kwa upande wa usajili wa magari na pikipiki, ada ya usajili gari utatoka kwenye shilingi 120,000 hadi kufikia 150,000 na pikipiki kutoka 35,000 hadi kufikia Shilingi 45,000

No comments:

Post a Comment