KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, June 10, 2010

Vikwazo zaidi dhidi ya Iran


Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura na kuamua kwamba nchi ya Iran inafaa kuwekewa vikwazo vipya, kutokana na kuendelea na mipango yake ya nguvu za nuklia.

Kura hiyo iliungwa mkono na nchi 12, kupingwa na mataifa mawili, na nchi moja ikiamua kutopiga kura, na kusubiri hadi raund yan nne ya vikwazo, ambavyo itakuwa ni kuiwekea nchi hiyo vikwazo zaidi vya kifedha na silaha.

Marekani inasema vikwazo vitakavyowekewa Iran ndio vitakavyokuwa vikali sana nchi hiyo imeshawahi kushuhudia.

Lakini hapo awali rais wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, alikuwa ameonya kwamba nchi yake haitakubali mashauri zaidi ya kuzungumzia juu ya nguvu za nchi hiyo za nuklia, ikiwa taifa lake litawekewa vikwazo.

Marekani na washirika wake wanadai kwamba Iran imo katika mipango ya kuunda bomu la nuklia, lakini serikali ya Tehran inasisitiza kwamba matumizi yake ya nguvu hizo ni salama.

Mapendekezo ya Baraza la Usalama kuiwekea Iran vikwazo yalikuwa yakipingwa na Uturuki na Brazil.

Lebanon ilijiondoa katika kura hiyo.

Vikwazo hivyo vimepitishwa baada ya upinzani wa Urusi na Uchina kupungua siku ya Jumanne.

No comments:

Post a Comment