KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 6, 2010

Uchaguzi mkuu Uingereza hii leo


LONDON

Wananchi wa Uingereza leo wanapiga kura katika uchaguzi mkuu unaonekana kuwa na ushindani mkubwa tokea mwaka 1992.Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema leo asubuhi.

Chama cha Conservative cha siasa za wastani za mrengo wa kulia, kinaongoza katika kura nyingi za maoni, lakini hakionekani kupata wingi wa viti vya bunge.Waziri Mkuu Gordon Brown ambaye anakabiliwa na ushindani mkubwa, anajaribu kukiongoza chama chake cha Labour , akiwania kipindi cha nne cha uongozi wa chama hicho.Hata hivyo kura nyingi za maoni hazimpi nafasi hiyo.

Chama kinachochukuliwa kuwa ni cha tatu kwa umarufu nchini Uingereza cha Liberal Democrats, huenda kikawa na turufu muhimu katika uchaguzi huo, kutokana na kuongezeka umaarufu wake na hivyo kuweza kupata viiti vingi.

Hali hiyo huenda ikalifanya bunge la Uingereza kushuhudia kutokuwepo kwa chama chenye wingi wa viti.Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa kutokuwepo chama kitakachopata wingi wa kuunda serikali , katika kipindi cha miaka takriban 40 iliyopita.

No comments:

Post a Comment