KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 6, 2010

Rais wa Nigeria afariki


Rais Umaru Yar´Adua amefariki.Rais huyo wa Nigeria amefariki akiwa na umri wa miaka 58, baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya moyo.Anatarajiwa kuzikwa hii leo.

Katibu wa Serikali kuu ya Nigeria Mahamoud Yayale Ahmed amesema kifo cha Rais Yar´Adua ni pigo kubwa kwa nchi hiyo.

Wakati huo huo, Kaimu rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan , ameapishwa hii leo kuwa Rais wa Nigeria kufuatia kifo hicho.

Jaji mkuu Aloysius Katsina-Alu alimuapisha bwana Jonathan kushika wadhifa huo, mpaka Mei mwakani mwisho wa kipindi cha urais cha hayati Yar´Adua, kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu.

No comments:

Post a Comment