KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 6, 2010

Ahukumiwa kifo kwa ugaidi Mumbai


MUMBAI

Mahakama nchini India leo imemuhukumu adhabu ya kifo raia wa Pakistan Mohammed Ajmal Amir Kasab, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika na mashambulio ya kigaidi mjini Mumbai mwaka 2008.

Jaji wa mahakama hiyo mjini humo, M.L.Tahaliyani alitoa adhabu hiyo ya kifo kutokana na makosa manne tofauti, ambayo ni mauaji,vita dhidi ya India, kula njama pamoja na ugaidi.

Hukumu hiyo ya kifo ambayo nchini India hutekelezwa kwa kunyongwa, hata hivyo itabidi ithibitishwe na mahakama kuu.

Mohammed Ajmal Kasab alikamatwa baada ya wenzake tisa kuuawa katika mashambulio hayo ya mwaka 2008 mjini Mumbai yaliyodumu kwa muda wa siku tatu, ambapo watu 166 waliuawa.

No comments:

Post a Comment