KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, May 7, 2010

Ramgoolam ashinda uchaguzi Mauritius


Kiongozi was upinzani Paul Berenger amekubali kushindwa katika uchaguzi wa wabunge Mauritius.

Matokeo yaliyothibitishwa yamempa waziri mkuu aliyepo madarakani Navin Ramgoolam wa chama cha Labour Alliance viti 41 vya ubunge kati ya 61 vilivyokuwa vinachuana.

Mwandishi wa BBC huko Mauritius anasema idadi kubwa ya watu walijitokeza kwa zaidi ya asilimia 70.

Mabadiliko ya kiuchumi na katiba, udanganyifu, rushwa, ulanguzi wa dawa za kulevya na ukabila ni baadhi ya mambo makuu katika uchaguzi huo.

Kumekuwa na mgawanyiko mkubwa baina ya Wahindu walio wengi nchini humo na wakristo, waislamu, chotara na watu wa Mauritania wenye asili ya kifaransa na kizungu.

Waziri mkuu Ramgoolam ni mfuasi wa dini ya Hindu na Bw Berengerni raia wa Mauritania mzungu, aliyekuwa wa kwanza kushika nyadhifa ya waziri mkuu katika kisiwa hicho asiye Mhindu mwaka 2003.

Mauritius huchukuliwa kuwa miongoni mwa nchi chache barani Afrika zenye mafanikio ya kijamii na kiuchumi.

Inafuata demokrasia ya kweli na imekuwa ikiongoza nchi hiyo kwa mujibu wa katiba kwa miaka mingi.

No comments:

Post a Comment