KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, May 6, 2010

Rais wa Nigeria Umaru Yar'Adua afariki


Rais wa Nigeria Umaru Musa Yar'Adua amefariki Dunia. Bw. Yar'Adua alifariki dunia saa tatu na nusu usiku wa Jumatano. Kiongozi huyo wa Nigeria alikuwa akiugua kwa muda mrefu. Kifo chake kilitangazwa na kituo cha televisheni cha Nigeria, N.T.A

Kwa mujibu wa taarifa ya kituo hicho, kifo cha Bw Yar'Adua kilitangwa na msemaji wa Ikulu, Ima Niboro. Kaimu wa rais Goodluck Jonathan aliarifiwa punde baada ya kifo hicho kutokea na kuelezea kuhuzunishwa sana na taarifa hizo.

Yar'Adua atazikwa Alhamis alasiri nyumbani kwake katika jimbo la Katsina.

Kiongozi huyo wa Nigeria alipatwa na maradhi ya ini mwaka 2000, lakini akapuuza taarifa kuwa hali yake ya afya ilikuwa mbaya. Yar'Adua alipelekwa nchini Saudi Arabia kwa matibabu mwezi Novemba mwaka jana. Tangu wakati huo hajaonekana hadharani.

Naibu wake, Goodluck Jonathan, alichukua hatamu za uongozi kama kaimu mnamo mwezi Februari, tayari ameapishwa rasmi kama Rais mpya wa Nigeria.

No comments:

Post a Comment