KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, May 13, 2010

MWanafunzi mmoja akamatwa

JESHI la POLISI mkoani Morogoro limefanikiwa kumkamata mwanafunzi mmoja kati ya sita waliohusika na mauaji ya mlinzi yaliyowafanywa na wanachuo wa chuo cha Sokoine cha Kilimo [SUA].

Mwanafunzi huyo ni Yona Mahona maarufu kama ‘Ngosha’ (29) anasoma shahada ya ufugaji wa samaki mwaka wa pili katika chuo hicho, ambaye alidaiwa kumpiga marehemu Jaffari Thabiti [38] aliyekuwa mlinzi chuoni katika sehemu zake za kichwani kwa kutumia kiti cha mbao na kumsababishia maumivu makali ambayo yalipelekea kifo chake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Thobias Andengenye alisema mwanafunzi huyo alikamatwa jana, majira ya mchana baada ya polisi kufika katika kampasi Mazimbu na kufanya upelelezi wa kina juu ya tukio hilo.

Alisema katika upelelezi huo polisi ulibaini kuwa mwanafunzi huyo akiwa na wenzake watano walihusiksa katika shambulio dhidi ya mlinzi huyo na kupelekea kupoteza maisha yake.

Alisema wanafunzi hao walimpiga mlinzi huyo kwakumtuhumu kuiba simu ya mkononi iliyokuwepo kwenye bweni la wanafunzi wa kike katika kampasi hiyo.

Hivyo jeshi hilo liko kwenye juhudi za kuwasaka na wengine waliohusika katka tukio hilo wawe kwenye mikono ya sheria.

No comments:

Post a Comment