KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 13, 2010

Daladalda zagoma- Morogoro


MADEREVA wanaotoa huduma ya usafirishaji kwa kutumia barabara ya Kata ya Mazimbu, Manispaa ya Morogoro wamegoma wakishinikiza kutengenezwa kwa barabara hiyo iliyokithiri ubobu wa hali ya juu.


Mgomo huo ulianzao jana kuanzia asubuhi umesababisha usumbufu mkubwa kwa abiria watumiayo barabara hiyo kushindwa kufika katka maeneo yao ya kazi kwa kukosa usafiri.

Mamia ya wananchi wanaotumia barabara hiyo kwa siku walililazimika kutembea kwa miguu ili kuweza kufika maeneo yao ya kazi na katika shughli zao za kila siku.

Wengine walionekanea kukodi pikipiki ambazo zilikuwa zinatoza kiasi cha shilingi elfu moja hali ambayo baadhi ya watu kushindwa gharama hiyo na kulazimika kut embea kwa miguu.

Mbali na yote wanafunzi ndio walionekana kuathirika zaidi na wengine kurudi majumbani kwa kuwa hawakuweza kumudu gharama hiyo ya pikipiki kuwafikisha mashuleni.

Mgomo huo wa madereva walidai wameufanya kwa kuudhiwa na manispaa kwa kushindwa kutengeneza barabara hiyo kwa muda mrefu kufikia hali ya kuharibu magari yao.

Madereva hao walisema zaidi kuwa barabara hiyo muhimu inayotumiwa na wahadhiri wa Chuo Kikuu SUA, wanafunzi pamoja na wananchi wa Kata hiyo wakiwemo wageni wa kimataifa imekuwa kero si kwao tu bali hata kwa abiria wenyewe na mgomo labda utaweza kuwashtua viongozi wa manispaa ili watengeneze barabara hiyo.


Barabara hiyo imeonekana kuwa na mashimo mengi na matope hali ambayo inafanya kuharibu magari yao na serikali husika kulifumbia macho suala hilo ili hali inaonekanea” walisema

“Ngoja tugome kwanza halafu wakiona wananchi weanahangaika wanaweza wakatengeneza, sisi tunatoa huduma kwa ananchi lakini mchango wetu hauonekani, magari yanaharibika kama unavyoona” walilalama

No comments:

Post a Comment