KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 6, 2010

Mitchell, Netanyahu kukutana tena leo

JERUSALEM

Mjumbe maalum wa Marekani katika mashariki ya kati, George Mitchell leo anakutana kwa mara ya pili na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika hatua ya kufungua njia ya kuanza kwa mazungumzo ya amani yasiyo ya ana kwa ana kati ya Israel na Palestina.

Viongozi hao walikutana kwa mara ya kwanza hapo jana.Bwana Mitchell, kabla ya kukutana tena na Waziri Mkuu Netanyahu, anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Israel Ehud Barak.

Hapo kesho mjumbe huyo wa Marekani katika Mashariki ya Kati anaonana na Rais Shimon Perez pamoja na kiongozi wa upinzani nchini humo, Bibi Tzipi Livni, kabla ya kuelekea ukingo wa magharibi katika mji wa Ramallah kwa mazungumzo na Rais wa mamlaka ya wapalestina Mahmaoud Abbas.

Afisa mmoja wa juu wa Palestina amesema, kamati kuu ya chama PLO siku ya Jumamosi inatarajiwa kukutana kuamua kuendelea na mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Israel, au la.

No comments:

Post a Comment