KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, May 6, 2010

Meli ya Urusi yakombolewa

MOSCOW

Manuwari ya kivita ya Urusi imefanikiwa kuikomboa meli ya mafuta ya nchi hiyo iliyotekwa na maharamia wa kisomali katika ghuba ya Aden, ikiwa na mabaharia 23.

Taarifa iliyotolewa mjini Moscow na mmiliki wa meli hiyo iitwayo MV Moscow University imesema kuwa mabaharia wote wamesalimika katika operesheni hiyo ya kuikomboa.Shirika la habari la Urusi limearifu kuwa katika operesheni hiyo haramia mmoja aliuawa na wengine kumi kukamatwa.Urusi imesema, maharamia hao waliyokamatwa watapelekwa nchini humo ili kushtakiwa.

Ofisi ya mwanasheria mkuu wa Urusi imesema kuwa utaratibu unaandaliwa kwa maharamia hao wa kisomali kusafirishwa hadi Urusi ambako watafunguliwa mashtaka kwa mujibu wa sheria ya nchi hiyo na ile ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment