KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 6, 2010

Kamati ya bajeti Ujerumani yaisaidia Ugiriki

BERLIN

Mpango wa serikali ya Ujerumani wa kuipiga jeki Ugiriki unatarajiwa kupitishwa bila ya kuungwa mkono na upande wa upinzani.

Hapo jana kamati ya bajeti ya bunge la Ujerumani, iliuridhia mpango huo wa miaka mitatu wenye thamani ya Euro bilioni 22.4, kwa kuungwa mkono na wajumbe kutoka vyama vinavyounda serikali vya CDU na FDP.

Wajumbe kutoka upande wa upinzani wa vyama vya SPD na kile cha kijani walisusia, huku wale wa chama cha mrengo wa shoto wakipiga kura ya kuukata mpango huo.

Maamuzi ya kamati hiyo ya bajeti ya bunge ni mapendekezo tu, kabla ya bunge kuupigia kura mpango huo hapo kesho.

Katika mjadala bungeni hapo jana upande wa upinzani, ulimshutumu Kansela Angela Merkel ukisema kuwa kuchelewa kwake kuiunga mkono Ugiriki kumeigharimu Ulaya mabilioni ya Euro.

No comments:

Post a Comment