KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, May 12, 2010

Maafisa wa soka wasimamishwa kazi Afrika Kusini

Maafisa wa ngazi ya juu wa shirikisho la Soka la Afrika Kusini wamesimamishwa kazi mwezi mmoja kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia.

Shirikisho la soka la Afrika Kusini Safa, limesema hakuna taarifa zaidi zitatolewa kuhusu tuhuma zinazowakabili wawili hao, hadi uchunguzi ufanyike.

gazeti moja la huko la Jumapili, lilichapisha taarifa inayodai kuwa mfanyabiashara moja wa Afrika Kusini ana miliki haki za nembo ya timu ya taifa ya nchi hiyo.

Hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na maafisa hao waliosimamishwa kazi.


Mashabiki wa soka Afrika Kusini

Meneja wa timu ya taifa Sipho Nkumane na mkurugenzi wa biashara wa Safa Victor Nosi, wamesimamishwa kazi huku wakisubiri utaratibu wa hatua za kinidhamu, Safa imesema katika taarifa yake.

"Ifahamike kuwa mpaka sasa hizo ni tuhuma tu dhidi ya maafisa hao, na uamuzi wowote utakaofuata utachukuliwa na taasisi za nje" imesema taarifa hiyo.

Safa imekuwa na mvutano mkubwa kati ya pande mbili zinazovutana ndani ya shirikisho hilo.

Kusimamishwa kazi kwa maafisa hao, hakutaathiri kazi ya kocha Carlos Alberto Pereira, au wachezaji wa timu ya taifa, maarufu kama Bafana Bafana.

No comments:

Post a Comment