KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, May 12, 2010

Waziri mkuu wa Uingereza ajiuzulu

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amejiuzulu rasmi wadhifa wa uwaziri mkuu.

Bw Brown amejiuzulu kufuatia kufanyika kwa uchaguzi mkuu ambao hakuna chama kilipata viti vya kutosha kuunda serikali. Baada ya kutangaza kujiuzulu bw Brown amekwenda kwa Malkia kuwasilisha waraka wake wa kujiuzulu.

Akitangaza hatua ya kujiuzulu akiwa na mkewe Sarah nje ya ofisi ya waziri mkuu 10 Downing Street, bw Brown amesema wadhifa huo ulikuwa "heshima kubwa" na kumtakia kila mema mrithi wake.

Uamuzi wake huo umekuja kufuatia chama cha Conservatives kukaribia kufikia makubaliano na chama cha Liberal Democrats. Bw Brown amesema alichukua uamuzi wa kujiuzulu baada ya kuona kuwa hatakuwa na uwezo wa kuunda serikali, baada ya siku kadhaa za mazungumzo kati ya vyama vya kisiasa kufuatia uchaguzi kumalizika bila ya mshindi thabiti.

Heshima kuongoza

Katika hotuba ya kujiuzulu iliyokuwa imejaa hisia bw Brown amesema "aliipenda kazi yake" na kuwa ilikuwa "heshima kubwa kuongoza".

"Niliipenda kazi yangu kwa kuwa na nafasi ya kuifanya nchi hii ninayoipenda kuwa bora na ya kidemokrasia" amesema Brown.

David Cameron anaelekea kwenda kuonana na Malkia.

No comments:

Post a Comment