KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, May 6, 2010

Bunge la Ugiriki kupiga kura

ATHENS

Bunge la Ugiriki, leo linatarajiwa kuupigia kura mpango wa hatua kali aza kubana matumizi zilizokubaliwa na serikali ya nchi hiyo wiki hii, ikiwa ni siku moja tu baada ya hapo jana watu watatu kuawa mjini Athens kufuatia ghasia za kuupinga mpango huo.

Hali katika mji huo mkuu wa Ugiriki, inaarifiwa kuwa shwari, baada ya siku mbili za mgomo wa nchi nzima.Watu hao watatu waliyouawa walikuwa ni wafanyakazi wa benki moja iliyochomwa moto na waandamanaji baada ya kutupa bomu la petroli ndani ya jengo la benki hiyo.

Katika hatua nyingine,vyama vikuu vya wafanyakazi nchini humo leo vimeitisha maandamano mapya kuupinga mpango huo wa serikali.

Serikali ya Ugiriki imelazimika kukubaliana na masharti ili kuweza kukopeshwa kiasi cha Euro billioni 110 na Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF.Masharti hayo ni pamoja na kubana matumizi, kuongeza kiwango cha kodi, na kuongeza umri wa kustaafu.

Hali hiyo tete nchini Ugiriki imeliathiri soko la fedha barani Ulaya na duniani kwa ujumla, ambapo sarafu ya Euro ilishuhudia ikishuka thamani huku Euro moja ikiwa sawa na dola moja na senti 29 za Marekani

No comments:

Post a Comment