KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, May 24, 2010

Inter mabingwa Ulaya waichapa Bayern 2-0


Historia ya ligi ya soka ya vilabu bingwa barani Ulaya imeandikwa upya baada ya Jose Mourinho kuiwezesha Inter Milan kuichapa Bayern Munich 2-0 na kutwaa taji kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 45.

Katika mechi hiyo iliyofanyika uwanja wa Bernabeu nchini Hispania, huku Bayern wakionekana kulegalega safu ya ulinzi, mshambuliaji Diego Milito kutoka Argentina alifunga magoli yote mawili kufanikisha ubingwa huo.

Kwanza aliipatia Inter goli la kuongoza alipomalizia vizuri mpira ulioanzia kwa mlinda mlango Julio Cesar ambaye alitanguliza mbele kujibu shambulio la Bayern.

Na alikamilisha ushindi kwa goli la pili, huku ngome ya Inter ikiwa imara kwa muda wote - matokeo hayo yameifanya Inter kuwa timu ya kwanza ya Italia kubeba vikombe vitatu vikubwa katika msimu mmoja.

Historia

Mafanikio yana maana kuwa, Mourinho, aliyeshinda kombe hilo akiwa kocha wa Porto mwaka 2004, anakuwa mtu wa tatu katika historia kushinda na vilabu viwili tofauti.

Anaungana na Ernst Happel na Ottmar Hitzfeld kupata heshma hiyo kubwa - akiwa ndiyo kwanza ana umri wa miaka 47, na kwa kufanya hivyo, amemaliza kiu ya miaka 45 ya Inter Milan kushinda tena taji kubwa zaidi katika soka ya vilabu Ulaya.

Jambo la muhimu zaidi ni kwa Mourinho ni kwamba amefanya hivyo akikabiliana na mwalimu wake Louis van Gaal, ambaye waliwahi kufanya kazi pamoja Barcelona kunako miaka ya 1990, na kuhitimisha mwanafunzi kumfunza mwalimu.

No comments:

Post a Comment