KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, May 24, 2010

Hali ya hatari yatangazwa Jamaica


Hali ya hatari imetangazwa katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu wa Jamaica, Kingstone baada ya vituo kadhaa vya polisi kushambuliwa na watu waliojihami kwa bunduki wakipinga kukamatwa kwa mlanguzi wa madawa ya kulevya.



Kituo kimoja cha polisi kiliteketezwa huku maafisa wa polisi wakiwafyatulia risasi washukiwa hao wanaodaiwa kuwa wafuasi wa mlanguzi huyo Christopher Dudus Coke anayesakwa na Marekani.

Wiki iliyopita serkali ya Jamaica iliahidi kumpeleka Bwana Coke nchini Marekani afunguliwe mashtaka ya ulanguzi wa madawa ya kulevya na kumiliki silaha kiharamu.

No comments:

Post a Comment