KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, May 11, 2010

Huku Mvua Ikinyesha, Mzee Yusuf Alamba Alamba Aaaamm...


Bendi Jahazi Modern Taarab ikiongozwa na Mzee Yusuf, "Mfalme" iliwapagawisha mamia ya watu waliojazana kwenye ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kwamba mvua nzito ilikuwa ikinyesha, washabiki wa taarabu badala ya kujibanza kwenye kona kujikinga na mvua, ndio kwanza spidi ya uchezaji wa miondoko ya Jahazi ilizidi kuwapagawisha.

Jahazi hivi sasa wanatamba na albamu yao mpya inayoitwa Daktari wa mapenzi ambayo ina jumla ya nyimbo sita.

Akiitambulisha albamu hiyo kwa washabiki wake, Mzee Yusuf alizitaja nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo kuwa ni Daktari wa mapenzi, wimbo ambao ndio unaobeba jina la albamu ukiwa umeimbwa na Mzee Yusuf mwenyewe.

Nyimbo zingine zilizomo kwenye albamu hiyo ni chokochoko Roho ya kwanini, Fungu la kukosa, Domokaya na ng'ombe wa masikini,

Mashabiki waliohudhuria shoo hiyo ya Jahazi hawakuweza kukaa chini huku akinadada wengi wakionyesha kupagawa kuliko kawaida wakimwaga radhi ukumbini kwa mauno yasiyo na mfano.

Gonga linki chini kujionea yaliyojiri ukumbini wakati Mzee Yusuf akipagawisha na "Alamba alamba Ammmmm....".

No comments:

Post a Comment