KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, May 11, 2010

TID na Ali Kiba Nani Mkali Kujulikana Jumapili


Nani mkali kati ya TID na Ali Kiba? Jibu litapatikana jumapili ya mei 2 baada ya shoo ya kukata na shoka itakayofanyika mjini Reading, Uingereza kwenye ukumbi wa Face Club.

Wasanii wote wawili wameweza kulifanya libeneke la Bongo Flava litambe kimataifa hali iliyowafanya wasanii hao wawe na tripu nyingi za kufanya shoo kwenye nchi za ulaya na Marekani.

Ali Kiba au kama anavyojulikana zaidi "Mzee wa Matonge" atapanda jukwaani kuonyesha makali yake dhidi ya TID (TOP IN DAR) katika usiku wa Banjuka Nite ambao umeandaliwa na DJ maarufu Uingereza, Richie Dee.

TID anatamba zaidi na nyimbo zake kama vile Zeze, Siamini, Watasema, Nyota Yangu, Asha wakati Ali Kiba atashuka na nyimbo zake kama vile Nakshi Nakshi, Mac Muga, Cinderella, Karim na Usiniseme.

Usiku wa Banjuka Nite utaanza saa nne usiku hadi saa 11 alfajiri.

Ukumbi wa Face Club upo mjini Reading, Chatham St, RG1 7JE

No comments:

Post a Comment