KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, May 24, 2010

Bilionea wa Nigeria Kuinunua Arsenal

Mfanyabiashara maarufu wa Nigeria bilionea Aliko Dangote amejitosa kwenye kuwania umiliki wa klabu kubwa ya Uingereza timu ya Arsenal ya jijini London.
Bilionea Aliko Dangote ambaye anakadiriwa kuwa na mshiko usiopungua dola bilioni 5, amejitosa kununua hisa za kuimiliki timu ya Arsenal ya Uingereza.

Aliko kwa kuanzia ametangaza kuzinunua shea za mmiliki namba nne wa Arsenal, mwanamama Nina Bracewell-Smith ambaye anamiliki asilimia 16 ya hisa za Arsenal.

Nina aliripotiwa na vyombo vya habari akisema kuwa ana mpango wa kuziuza hisa zake za Arsenal kwa paundi milioni 160 hali iliyosababisha bilionea huyo wa Nigeria aamue kujitosa kuzinunua.

Hatua ya bilionea huyo wa Nigeria kuzinunua hisa za Arsenal itasababisha vita vya umiliki wa Arsenal viwe vikubwa kati ya bilionea huyo na mabilionea wawili wenye kumiliki hisa nyingi zaidi za Arsenal, bilionea Stan Kroenke na bilionea wa urusi Alisher Usmanov.

Aliko ambaye ni shabiki mkubwa wa Arsenal inaaminika kuwa ana uwezo wa kipesa wa kupimana ubavu na mabilionea hao wa Arsenal katika kuwania kuimiliki timu hiyo kubwa ya kaskazini mwa jiji la London.

Aliko amekuwa kwenye ukanda wa soka nchini Nigeria kwa muda mrefu na amekuwa akiifadhili kifedha timu ya taifa ya soka ya Nigeria

No comments:

Post a Comment