KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, May 24, 2010

Mahubiri yalimfanya Nasib ajaribu kulipua Ubalozi

KATIKA mahojiano yanayoendelea kati ya maofisa wapelelezi ya kumuhoji mwanafunzi Nasibu yamebaini kuwa mwanafunzi huyo alishawishika kutaka kulipua ubalozi kutokana na mahubiri ya Shekhe wa Msikiti wa Mtambani wa Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Naibu Kamishna wa Polisi, Peter Kivuyo alisema kuwa, katika mahojiano yao na mwanafunzi huyo alikiri kuwa alikuwa na nia ya kulipua ubalozi huo tangu mwishoni mwa mwaka jana baada ya kusikia mahubiri kutoka kwa sheikh asiyemtambua jina wa Msikiti huo wa Mtambani.

Katika maelezo ya Kamishna huyo ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini alisema, mahubiri hayo aliyoyasikia mwanafunzi huyo kutoka kwa muhubiri huyo yalimjengea chuki kuwa majeshi ya marekani yanawaua Waislamu wasio na hatia.

Kivuyo alisema kuwa mwanafunzi huyo alikiri kuwa alikuwa na nia ya kulipua ubalozi huo tangu mwishoni mwa mwaka jana 2009, baada ya kusikia mahubiri kutoka kwa sheikh wa Msikiti huo ambaye hamfahamu jina.

Katika ufafanuzi huo ulisema, Nasib alifika nje ya ubalozi huo Mei 16, mwaka huu katika eneo la sehemu yanakoegeshwa magari ya maji na kurusha chupa iliyokuwa na mafuta ya taa na utambi ambavyo havikuleta madhara yoyote.

Alirusha chupa ya mafuta ya taa na chupa hiyo ilifika kwenye lori la maji lililoegeshwa kenye ukuta wa ubalozini humo” alisema

Alisema kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa ndani ya ubalozi huo ilisema kuwa, chupa hiyo ilipasuka lakini haikulipuka wala kuwa na madhara, ambapo mtoto huyo baada ya kuona hivyo aliamua kurusha chupa ya pili, ambapo hata hivyo hakufanikiwa baada ya walinzi waliokuwa lindoni ubalozi hapo kumkamata.

Wanafunzi hao wawili bado wanaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.

No comments:

Post a Comment