KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, May 11, 2010

Ali Choki na Kupaza Kukumbushia Enzi Zao


Akizungumza na Nifahamishe, Kupaza ‘Mwana Tanga’ alisema kuwa wameamua kuungana kutoa albamu hiyo kwa lengo la kuutambulisha muziki asili wa Kitanzania na kujaribu kuutafutia soko.

“Unajua sisi tumekaa chini na kuangalia ni namna gani tunaweza kuutambulisha muziki wa asili wa Tanzania, tukaona ni vyema tukakaa chini na kufanya kazi hii ambayo tunaamini itasaidia,” alisema Kupaza.

Kupaza anasema kuwa yeye na Choki ni wanamuziki wenye majina makubwa na yanayokubalika, kwa hiyo watakapofanya kazi hiyo, itakuwa ni rahisi kwa wanamuziki wengine vijana kufuata njia.

“Wengi wanasema muziki wa asili hauna soko. Lakini nadhani tatizo si soko, tatizo ni nini unachofanya. Sasa sisi tunataka kuonyesha njia ili wengine wafuate na kuanza kuuenzi muziki wa asili,” alisema Kupaza.

Kupaza alisema kuwa tayari maandalizi ya kazi hiyo yameshaanza na kilichobaki sasa ni kusubiri uzinduzi wa Extra Bongo upite ili waweze kukaa chini na kuifanya kazi hiyo kikamilifu.

“Hivi sasa Choki anajiandaa na uzinduzi wa bendi yake ya Extra Bongo, sasa tunasubiri atakapomaliza tunaingia msituni rasmi kufanya kazi," alisema Kupaza

No comments:

Post a Comment