KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, March 6, 2010

Terry ashukuru mashabiki kumuunga mkono
John Terry alijisikia ameungwa mkono vizuri na mashabiki wa soka wa England katika mchezo wa Jumatano wa kirafiki walipoifunga Misri mabao 3-1 katika uwanja wa Wembley.
Terry aliichezea England kwa mara ya kwanza tangu alipopokonywa unahodha baada ya tuhuma za kuwa na uhusiano na aliyekuwa mpenzi wa Wayne Bridge.

Nahodha huyo wa Chelsea, amesema amefurahishwa na namna mashabiki walivyomuunga mkono na amewashukuru.

Ameongeza kusema kulikuwa na watu wachache waliozomea mwanzoni lakini ameweza kuyadhibiti. Wana haki ya kutoa mawazo yao.

Kulikuwa na wasiwasi Terry, aliyekuwa akizomewa na mashabiki wa timu za upinzani katika michezo ya Ligi Kuu ya England hivi karibuni, angekuwa na wakati mgumu katika uwanja wa Wembley, hali iliyomfanya Wayne Rooney kuwaomba mashabiki kutomzomea.

No comments:

Post a Comment