KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, March 6, 2010

Waziri Mkuu Brown ahojiwa kuhusu Iraq


Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown ameliambia jopo linalochunguza uvamizi wa Iraq kwamba uamuzi wa kuishambulia nchi hiyo ulifanywa kwa sababu za msingi.
Akihojiwa moja kwa moja kwenye runinga mjini London, Gordon Brown amesema akitegemea taarifa za vyombo vya ujasusi aliamini kwamba Iraq ni tishio la kukabiliwa na kuwa mpango wa utulivu kimataifa ulikuwa hatarini.

Bw Brown, ambaye wakati huo alikuwa waziri wa fedha chini ya serikali ya Tony Blair, amekanusha habari kuwa kulikuwepo na upungufu katika vifaa vya majeshi kutokana na uhaba wa fedha.

No comments:

Post a Comment