KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, March 6, 2010

Stuart Holden wa Bolton avunjika mguu
Kiungo wa Bolton Stuart Holden hataweza kucheza soka kwa wiki sita baada ya kuvunjika mguu wake wa kulia.
Holden alijeruhiwa wakati akichezea Marekani iliyofungwa mabao 2-1 na Uholanzi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa siku ya Jumatano.

Holden mwenye umri wa miaka 22 aliyejiunga na Bolton mwezi wa Januari, alicheza tangu mwanzo katika klabu yake mechi mbili zilizopita dhidi ya Wolves na Tottenham.

Nae meneja wa Bolton Owen Coyle ameeleza katika mtandao wa klabu hiyo, katika mechi zote mbili aligundua kipaji cha mchezaji huyo, kwa hiyo kuumia kwake ni pigo kubwa. Aliongeza kusema jambo la muhimu atarejea imara zaidi.

No comments:

Post a Comment