KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, March 3, 2010

Serikali ya mpito yaundwa Niger


Serikali ya mpito yaundwa Niger

Viongozi wa kijeshi nchini Niger wameunda serikali ya mpito inayojumuisha mawaziri 20 wakiwemo wanajeshi watano na wanawake watano.
Serikali hii imeundwa wiki mbili tu baada ya jeshi kupindua serikali ya Rais Mamadou Tandja.

Kwa mujibu wa redio ya taifa, wizara za ulinzi, michezo na mazingira zimekabidhiwa majenerali watatu walio na uhusiano wa karibu na Rais aliyepinduliwa.

Kiongozi mpya wa kijeshi, Meja Salou Djibo, ameahidi kurejesha Niger katika mfumo wa demokrasia ingawa hajaeleza tarehe kamili.

Rais Tandja aling'olewa mamlakani baada ya kubadilisha katiba ya nchi ili kumruhusu kusalia mamlakani hata baada ya muhula wake wa pili anaoruhusiwa kikatiba kukamilika.

No comments:

Post a Comment