KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, March 3, 2010

Mchezaji wa Man City matatani
Mchezaji wa Manchester City anachunguzwa kufuatia tuhuma za kumpiga kichwa shabiki wa Manchester United katika kilabu cha pombe cha usiku.
Michael Johnson anatuhumiwa kwa kumpiga shabiki huyo aliyekuwa akiimba nyimbo za Manchester United mtaa wa 42 katikati ya Manchester city mwezi wa Desemba.

Johnson, mwenye umri wa miaka 22, baadae alikamatwa kwa tuhuma za kudhuru na kumsababisha maumivu mtu aliyempiga.

Msemaji wa polisi amesema mchezaji huyo yupo nje kwa dhamana hadi tarehe 14 mwezi wa Aprili.

Polisi wamesema watu wengine wawili pia wamehojiwa.

No comments:

Post a Comment