KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, March 3, 2010

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amezuru eneo kulikotokea mkasa wa maporomoko ya ardhi


Rais Yoweri museveni awafariji waathiriwa

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amezuru eneo kulikotokea mkasa wa maporomoko ya ardhi mashariki mwa nchi hiyo. Inahofiwa kuwa zaidi watu 300 wamekufa.
Mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha katika eneo hilo lenye milima la Bududa ndio imelaumiwa kuwa kwa kusababisha janga hilo.

Waziri wa Uganda anayeshungulikia majanga, Tarsis Kabwegyere, amesema kuwa bado hawana picha kamili ya athari za janga hilo.

Mkurugenzi wa shirika la msalaba mwekundu nchini humo, Michael Nataka, anasema shughuli za uokozi zingali zinanedelea na shirika hilo linaomba msaada zaidi.

Kwa mujibu wa shirika hilo maiti themanini zimepatikana huku watu arobaini wakiokolewa. Zaidi ya watu 250 bado hawajulikani waliko.

No comments:

Post a Comment