KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, March 3, 2010

Fedha za msaada zilinunuliwa silaha Ethiopia




Shirika la utangazaji la BBC limepata ushahidi kuwa mamilioni ya dolla kwa ajili ya msaada ili kukabiliana na hali ya ukame nchini Ethiopia mnamo miaka ya themanini zilitumika kununulia silaha.
Ukame uliotokea wakati huo uliwafanya watu millioni saba kuwa katika hali ya kuhitaji msaada wa dharura, huku dunia nzima ikitawaliwa na picha za baa la njaa, na watu walioonekana kukata tamaa.

Juhudi kubwa za kutafuta msaada, zilizo-ongozwa na mwanamuziki wa mtindo wa rock Bob Geldof, zilikusanya fedha nyingi ambazo hazikutarajiwa.

Wakati huo mashirika ya misaada yalilazimika kufanya kazi pamoja na waasi ili kuwafikia waathiriwa wa baa hilo la njaa.

Mmoja wa viongozi wa waasi alisema ni asilimia tano tu ya fedha hizo ambazo zilitumika kwa ajili ya kupambana na janga hilo la ukame.

No comments:

Post a Comment