KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, March 3, 2010

Meli ya Saudi yatekwa Ghuba ya Aden


Maharamia wa kisomali wameiteka nyara meli kubwa ya Saudia katika ghuba ya Aden.
Meli hiyo, Al Nisr Al Saudi, ilikuwa na mabaharia 14 lakini haikuwa imebeba mafuta.

Nahodha wa meli hiyo ni raia wa ugiriki ma mabaharia wengine wanaamika kuwa raia wa Sri Lanka.

Kwa mujibu wa wanajeshi wa majini kutoka ulaya wanaoshikika dorioa katika eneo hilo, maharamai wa kisomali wanashikilia meli 6 na mabahararia 132.

Visa vya utekaji meli katika ghuba ya Aden huongezeka katika miezi ya Machi , Aprili na May kwa sababu ya hali mbaya ya anga.

No comments:

Post a Comment